RIWAYA MPYA YENYE KILA AINA YA MAUDHUI MADHUBUTI KATIKA JAMII ZETU MBALIMBALI iliyotungwa na mtunzi mahiri
Prince Kalonga
Author;
Prince Kalonga
Book/ novel ; OLE! ADUI WA HERI
Year ; 2013/ 2014
Publishers; Printing press Dar es Salaam
SURA YA KWANZA
Ulikuwa ni wakati mtulivu, wakati wa mapambazuko na
kwa mbali upande wa mashariki lilionekana jua likichungulia taratibu
mithili ya uyoga unaochoza toka ardhini. Ndege, wadudu na viumbe
wengine walionekana wakirukaruka huku na huko ili kutafut a riziki zao.
Jua nalo bila kisita liliendelea kudhiharisha umahali wa nuru yake
katika kuiangaza dunia yote. Sasa ulikuwa umewadia wakati wa chifu
Katitu kwenda mawindoni kama kawaida yake. Chifu katitu alikuwa ni chifu
maarufu kati ya machifu waliokuwa wakiongoza miji ya jirani. Chifu
Katitu alikuwa akiongoza mji uitwao Zembilye
Mara kwa mara Chifu Katitu aliweza kuamka asubuhi na mapema na kuandaa
zana zake alizokuwa akizitumia katika mawindo pamoja na mbwa wake
watano. Baada Chifu Katitu kuamka na kuandaa zana zake kama vile upinde
, mishale ishirini iliyosheheni kwenye kwenye podo lake kubwa ambalo
alilining’iniza nyuma ya mgongo wake, panga na manati yaliyokuwa
yametengenezwa na mtaalam tokea kijijini hapo.
Mbwa wa Chifu Katitu walitunzwa na kupewa mafunzo ya hali ya juu kwa
ajili ya mawindo, Mbwa hawa walimsaidia sana chifu Katitu katika
lkazi yake ya uwindaji, Mbwa wa chifu Katitu walikuwa mbwa hodari sana
kutokana na kuwa n afya nzuri pia kupew mafunzo maalum kwa ajili ya
uwindaji. Mbwa walimsaidia katika kazi ya kufukuza wanyama , kuwatisha
na hata pia kuwakamata, kitu cha zaidi walichofundishwa hawa mbwa
ilikuwa ni kutokula nyama ya mnyama waliyemkamata mpaka pale
watakapoluhususiwa na bwana wao ambaye alikuwa ndiye chifu Katitu
Baada ya kuandaa zana na mbwa wake, Chifu Katitu
aliwaaga wake zake, chifu Katitu alikuwa na wake watatu, mke mkubwa
aliitwa Mwansome, Huyu alikuwa ni mke wa kwanza kuolewa na chifu Katitu
na pia alibahatuka kupata watoto wawili. Mke wa pili aliitwa Chambiso,
Huyu alikuwa mke wa pili kuolewa na chifu Katitu. Chambiso hakubahatika
kupata mtoto. Mke wa tatu alifahamika kwa jina la Bwinsyeho, huyu
alikuwa mke mdogo na mke wa tatu kuolewa na chifu Katitu kati ya wake
aliokuwa nao, Huyu nae alibahatika kupata watoto wawili.
Baada ya chifu Katitu kuwaaga wake zake, alianza safari ya
kwenda msituni akiwa na watumishi wake waaminifu na pia walikuwa hodari
kwa shughuli mbalimbali katika utawala wa chifu Katitu , zikiwemo
shughuli za mapigano katika jeshi na shughuli za uwindaji. Kutokana na
uaminifu na jitihada zao, Chifu Katitu aliweza kuwapa kipaumbele katika
kazi mbalimbali za muhimu katika utawala wake, mfano katika mapambano
na maadui wa miji jirani, Chifu Katitu aliweza kuwaweka kama viongozi
wa vikosi mbalimbali vilivyokuwwa vikienda kupigana na miji iliyokuwa
inajaribu kuvamia mji wa Zembilye
Watumishi hodari
wa chifu Katitu walifahamika kwa majina kama Chamaka , Yonzebo na
Gambiro na pia watumishi hawa kutokana na uhodari wao na uaminifu chifu
Katitu aliwaweka kuwa walinzi wake pale alipokuwa nyumbani na hata
anatoka kwenda sehemu mbalimbali kama porini kwa ajili ya kuwinda,
kwenye vikao na wazee wa kijijini hapo na hata alipoalikwa kwenye
sherehe mbalimbali nje ya mji wake
*************************
Zembilye ulikuwa ni mji maarufu sana kiliko miji yote
iliyokuwa mpakani mwa mji huu. Umaarufu wa mji wa Zembilye ulitokana na
jitihada kubwa za wananchi wake katika kufanya shughuli mbalimbali za
maendeleo na ushirikiano wa wanazembilye katika kutekeleza majukumu
hayo ya kijiji na mji wao kiujumla.
Mji wa Zembilye
pia uliweza kufahamika na kuwa maarufu kutokana na ubora wa miundombinu
yake katika vijiji vilivyokuwa vinapatikana ndani ya mji wa Zembilye.
Wanakijiji waliweza kushirikiana katika kutengeneza barabara kubwa
zilizokuwa zikiwasaidia katika kusafirisha mazao mbalimbali na nafaka
nyingi toka mashambani mwao na kuyapeleka kwenye maghala, majumbani mwao
na hata pia sokoni pale kulipokuwa na uhitaji wa fedha. Pia Zembilye
ulikuwa mji uliosifika kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali kama vile
ng’ombe wa maziwa na nyama , mbuzi wa maziwa na nyama, kondoo, kuku,
nguruwe, punda na bata. Ufugaji wa mifugo hii uliwafanya wakulima wa
mji wa Zembilye kufanya kazi zao kwa urahisi kama kulima na kubeba
mizigo mbalimbali na pia mbolea ya asili iliyofahamika kama samadi, hii
ilitokna na kinyesi cha wanyama ambayo wakulima waliitumia kama mbolea
wakati wa kupanda mazao na kuwasaidia kuvuna mazao mengi na bora.
Wanyama hawa licha ya kuwa na faida kemkem pia waliweza kuuzwa na fedha
zilizopatikana zilitumika katika kufanyia shughuli zingine mbalimbali
za kimaendeleo
Jeshi imara la mji wa Zembilye ni
moja kati ya vitu viliivyoupatia mji umaarufu sehemu kubwa na nyingi
pembezoni na mbali ya miji jirani, hii ilitokana na ushindi wa mara kwa
mara uliokuwa unapatikana pale walipokuwa wakienda katika vita. Jeshi
hili lilikuwa na askari hodari wenye nguvu , ushirikiano na umoja
katika shughuli mbalimbali za kijeshi na pia lilikuwa ni jeshi
lililokuwa likifanya mazoezi bora kwa ajili ya kujiimarisha katika vita
na mapigano yao na maadui zao, Mazoezi yaliyokuwa yamepewa kapaumbele ni
kama vile kurusha mikuki kwa mkono, kutumia pinde kurusha mishale ,
kutumi rungu na mitaimbo
Miji iliyokuwa jirani
na mpakani kuuzunguka mji wa Zembilye ilijaribu kutumia kila njia ili
kuuvamia mji wa Zembilye lakini “waligonga mwamba”. Chifu Katitu nae
aliweza kujigamba waziwazi mbele ya miji jirani iliyokuwa inauzunguka
mji wake, Alifanya hivi kutokana na kuwa na jeshi imara lililokuwa
likifanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa. Kambi ya jeshi na makao makuu
ya jeshi yalikuwa karibu na makazi ya chifu Katitu
*********************************
Taratibu ukubwa wa nyumba za kijijini ulianza kupungua kwa
muonekano kutokana na safari ilivyokuwa ikizidi kusonga mbele.
Hatimaye wakaanza kuzitazama nyumba za kijijini mithili ya kuchungulia,
Hali hii ilionyesha dhahiri umbali waliotembea toka kijijini na wimgi
wa miti pale walipoanza kuingia porini. Pori hili lilikuwa jirani
kabisa na mji wa Zembilye. Walipozidi kusonga kusonga mbele kidogo
waliona kijito kidogo mithili ya mfereji. Kamto haka kalikuwa na maji
masafi sana ambayo yalitumika katika kunyweshea mifugo pale ambapo
wachungaji wa mifugo walileta mifugo yao katika pori lile, lakini nao
pia waliweza kutumia yale maji kwa ajili ya kunywa. Kamto haka kalikuwa
na faida kubwa sana kwa wanakijiji hasa wakati wa kiangazi. Hakakuweza
kukauka kutokana na wingi wa mito iliyokuwa imesheheni katika msitu ule.
Wanakijiji wa mji wa Zembilye walikaweka kakijito haka kama akiba yao
ya maji pale ilipotokea shida ya maji wakati wa kiangazi, kwani wakati
wa kiangazi visima vya wanakijiji vingi na mito iliyokuwa kijijini
iliweza kukauka kutokana na jua kuwaka sana kwa mda mrefu.
***********************
Chufu Katitu alipofika kwenye kajito kale alichota
kiasi cha maji na kuyaweka katika mifuko ya ngozi ya ng’ombe iliyokuwa
imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuwekea maji na hata pia maziwa,
ilitengenezwa kwa kutumia ngozi laini iliyoandaliwa kitaalamu.
Wote walichota maji kwa ajili ya kutumia katika safari
yao pale ombapo wangepatwa na kiu au uchovu wa safari.
Baada ya kuchota maji chifu Katitu aliziruhusu mbwa zake zinywe
maji, Mbwa walipomaliza kunywa maji, chifu Katitu pamoja na watumishi
wake waliendelea na safari yao.
Baada ya safari
ndefu kidogo waliweza kuona kichaka kwa mbali kikitikisika, ndipo chifu
Katitu alipowaamuru watumishi wake watulie kimya na wachukue tahadhari
kwa lolote litakalotokea. Lakini kutokana na uzoefu wa chifu Katitu
katika kazi yake ya uwindaji aliweza kugundua kuwa katika kichaka kile
panaweza kuwa na kanga wanaotaga mayai wasiopungua watatu, kwani
kutokana na kugombania sehemu ya kutagia ndipo husababisha vurugu na
kupelekea kichaka kutikisika.
Chifu Katitu na
watumishi wake walianza kujongea taratibu kuelekea uelekeo wa kichaka.
Chifu Katitu aliwaambia watumishi wake kwa kunong’ona “njoo tukizunguke
kichaka hiki ili kanga wasipate nafasi ya kukimbia”. Walipokizunguka
kile kichaka kwa haraka na uhodari mkubwa wote waliruka na kutia mikono
yao katikati ya kichaka kile, kwa bahati nzuri waliweza kukamata kanga
wawili wakubwa na kama chifu Katitu alivyohisi kweli palikuwa na kanga
watatu mmoja alifanikiwa kuruka juu na kutokomea mbali. Lakini kwa
bahati mbaya walipokuwa wanaluka kuelekea kuelekea kwenye kichaka,
mtumishi mmoja wa chifu Katitu aliyeitwa Yonzebo ilichomwa na mwiba
mkubwa uliofahamika kwa jina la mchongoma, alichomwa sehemu ya unyayo
wake katika mguu. Harakaharaka Yonzebo alitafuta mgomba pori na
kuchukua kamba zilizotokana na mgomba huo kasha akajifunga sehemu ile
iliyokuwa imepatwa na jeraha ili kuzuia damu isiendelee kutoka.
Baada ya Yonzebo kupatiwa huduma hii ya awali chifu Katitu alitoa
mfuko mmoja uliokuwa umetengenezwa kwa kutumia nyuzi za katani,
Kisha akawaweka wale kanga pamoja na mayai sitini yaliyopatikana
kwenye kichaka kile, baada ya kuweka katika mfuko alimpatia Chamaka
aubebe mfuko uliokuwa umewekwa kanga pamoja na mayai
Waliendelea na safari yao kuelekea ndani zaidi ya msitu mnene
uliosheheni kila aina ya mimea na maua yenye harufu nzuri tena
mbalimbali na muonekano tofautitofauti unaovutia na usiovutia machoni
pa binadamu na wanyama pia.
Katika msitu huu
walipatikana wadudu wa kila aina , wanyama mbalimbali wakubwa na wadogo
kama vile sungura, cheche, nyati, samba, swala na hata pia panya
walipatikana na kila kiumbe ambaye aliweza kustahili kuishi katika
mandhali yam situ ule. Hakika pori hili lilikuwa ni msitu mkubwa
uliokuwa na kila aina ya kiumbe aliyestahli kuishi msituni.
SURA YA PILI
Wake wa chifu Katitu walipendana sana bila kujari utofauti
wao, Wake hawa waliishi kwa furaha. Mke wa pili ambaye hakufanikiwa
kupata mtoto aliweza kuwatuma watoto wa wake wenza katika kazi
mbalimbali na pia hata hawa watoto licha ya kuwa Chambiso si mama yao
lakini walimtii na kumuheshimu kama walivyokuwa wakiwaheshimu mama zao.
Wake wa chifu Katitu mara nyingi walikaa pamoja huku
wakiimba pale walipokuwa wamemaliza shughuli zao mbalimbali.
Walisaidiana katika kazi za shambani, hata wanakijiji walisifu na
kupenda jinsi wake wa chifu wao Katitu walivyokuwa wanaishi kwa
kupendana na ushirikiano na kuishi kwa raha, licha ya kuwa na furaha na
amani, kulikuwa na vikwazo vilivyotolewa na me wao chifu Katitu. Chifu
Katitu hakumpenda mke wa pili, kutopendwa kwa Chambiso kulitokana na
kutozaa mtoto hata mmoja tangu aolewe na bwana wake chifu. Kutokana na
sababu hii chifu Katitu aliwapenda sana wake wawili mke mkubwa na mke
mdogo bkwa sababu walimpatia watoto. Chifu Katitu aliweza kufikia
hatua ya kumpiga na kumtukana mkewe wa pili pale tu alipofanya kosa
dogo tu, Lakini kutokana na upendo waliokuwa nao wake wa chifu Katitu
waliweza kumfariji mwenzao pale tu aliposababishiwa huzuni mme wao na
pia walimtia moyo na kumpa tumaini kwamba ipo siku mungu atamsaidia na
atabahatika kupata motto na shida zote anazozipata toka kwa chifu
Katitu zitatoweka. Chambiso alionekana mtu mwenye furaha siku zote
kutokana na kufarijiwa na wake wenzake, hakujari shida anazopata toka
kwa mumewe.
Wake wa chifu Katitu walikuwa na hekima
isiyokifani, kutokana na hekima yao waninchi hawakusita kupeleka
matatizo yao pale ambapo chifu Katitu alipokuwa mbali na himaya yake
ndani ya mji wa Zembilye. Kwa ufanisi mkubwa wake wa chifu Katitu
waliweza kutatua matatizo ya wakazi wa mji wa Zembilye. Utatuzi huu
ulikuwa rahisi kutokana na udogo wa matatizo ya wnanchi wa Zembilye,
matatizo hayo kama wizi mdogomdogo na ugomvi kati ya wanandoa na
wanakijiji.
***************************
“Bhooooooooo!!........... bhoooooooooo!!................
bhooooooooo!!................” huu ilikuwa ni sauti ya mnyama
iliyosikika mita chache toka sehemu waliyokuwepo wawindaji hawa hodari
baada ya kutembea kilomita kadhaa toka kwenye kijito ambacho waliweza
kuchota maji ya kunywa. “Shiiiiii, shiiiiii, shiiiiii” hiii ilikuwa ni
amri na ishara toka kwa chifu Katitu ikwaamuru watumishi wakae kimya.
Ndipo wakaanza kujongea taratibu kuelekea kule sauti ilikosikika,
Walitembea mithili ya watu wanaotembea ndani ya jumba bovu lisilohitaji
bugudha wakihofia kuangukiwa na jumba hilo. Walitembea kimya bila sauti
ya aina yoyote kusikika kwani walikuwa wazoefu na kazi hii ya
uwindaji.
Kutokana na udhoefu wa chifu Katitu katika
uwindaji na watumishi wake, waliweza kuzifahamu aina mbalimbali za sauti
za wanyama. Uzoefu huu uliwafanya watambue sauti iliyokuwa imesikika
punde, ilikuwa ni sauti ya nyati dume. Kutokana na sifa za wanyama,
mmnyama waliyemsikia akipiga kelele aliwafanya wachukue tahadhari ya
hali juu. Safari hii Chamaka ndiye aliyekuwa akiwaongoza wenzake mithili
ya bata na watoto wake, tofauti na mwanzo pale walipokuwa wanaanza
kuingia msituni, kwani hapo awali chifu Katitu ndiye aliyekuwa akiongoza
wenzake katika safari yao. Taratibu walisogea mbele kuelekea sehemu
ambayo sauti ya mnyama ilisikika, wapili kufuatia katika mstari alikuwa
ni chifu Katitu, Gambiro na Yonzebo, Yonzebo alikuwa wa mwisho kwa
sababu ya jeraha alilokuwa nalo mguuni katika unyayo, jeraha ambalo
lilimfanya awe dhaifu kwa kiasi Fulani katika mawindo
“Kwachu, kwachu, kwachu” nisauti iliyosikika na wawindaji hawa
hodari katika msitu. Sauti hii ilisikika umbali Fulani mita kadhaa
kutoka kwenye kichaka mbele yao. Kichaka hiki kilikuwa kimestawi vizuri,
kikiwa na majani mabichi yaliyovutia kwa chakula cha wanyama wote wala
majani. “Jitayarishe” Harakaharaka utekelezwaji wa sauti hii ulianza
kutendeka, ilikuwa ni sauti ya chini iliyotamkwa na Yonzebo huku hofu
ikimjia kwa mbali kutokana na udhaifu alionao. Alitamka kauli hii baada
ya kuona mkia mkubwa wa nyati uliokuwa ukilushwa hewani huku na huko
Uwindaji wa chifu Katitu ulikuwa ni uwindaji wa hali
ya juu uliokuwa na kila aina ya mbinu bora za uwindaji, Mara nyingi
walifanikiwa katika mawindo yao. Mafanikio hayo yalitokana na mbinu
mojawapo waliyokuwa wakiitumia sana mawindo yao, Mbinu hii ilikuwa ni
mbinu ya kulusha mikuki au mishale yao kwa pamoja wakikusudia kumpata
mnyama yoyote waliyemkusudia kwa wakati huo. Mbinu hii ilitumika mara
kwa mara na tena mara nyingi kutokana na kuwa na mafanikio makubwa
katika kazi yao ya uwindaji.
Walipokuwa tayarib
katika upande wa zana zao kuelekea kule alipokuwepo mnyama, walitega
masikio kumsikiliza chifu Katitu. “Moja, mbili, tatu” hii ilikuwa ni
sauti ya chifu Katitu ambayo hatima yake ilikuwa ni kuwaruhusu watumishi
wake kurusha mishale kutoka kwenye pinde zao kwa pamoja kuelekea
uelekeo wa mnyama. Mara tu alipomaliza kuhesabu, mishale ilichoka kwenye
pinde zao kwa kasi ya ajabu..................................ITAENDELEA
kwa maoni na ushauri, ufadhili, ntafute kwa
NO ; 0653081338 /
Email ;
princekalonga22gmail.com