RIWAYA MPYA YENYE KILA AINA YA MAUDHUI MADHUBUTI KATIKA JAMII ZETU MBALIMBALI iliyotungwa na mtunzi mahiri Prince Kalonga
Author; Prince Kalonga
Book/ novel ; OLE! ADUI WA HERI
Year ; 2013/ 2014
Publishers; Printing press Dar es Salaam
SURA YA KWANZA
Ulikuwa ni wakati mtulivu, wakati wa mapambazuko na kwa mbali upande wa mashariki lilionekana jua likichungulia taratibu mithili ya uyoga unaochoza toka ardhini. Ndege, wadudu na viumbe wengine walionekana wakirukaruka huku na huko ili kutafut a riziki zao. Jua nalo bila kisita liliendelea kudhiharisha umahali wa nuru yake katika kuiangaza dunia yote. Sasa ulikuwa umewadia wakati wa chifu Katitu kwenda mawindoni kama kawaida yake. Chifu katitu alikuwa ni chifu maarufu kati ya machifu waliokuwa wakiongoza miji ya jirani. Chifu Katitu alikuwa akiongoza mji uitwao Zembilye
Mara kwa mara Chifu Katitu aliweza kuamka asubuhi na mapema na kuandaa zana zake alizokuwa akizitumia katika mawindo pamoja na mbwa wake watano. Baada Chifu Katitu kuamka na kuandaa zana zake kama vile upinde , mishale ishirini iliyosheheni kwenye kwenye podo lake kubwa ambalo alilining’iniza nyuma ya mgongo wake, panga na manati yaliyokuwa yametengenezwa na mtaalam tokea kijijini hapo.
Mbwa wa Chifu Katitu walitunzwa na kupewa mafunzo ya hali ya juu kwa ajili ya mawindo, Mbwa hawa walimsaidia sana chifu Katitu katika lkazi yake ya uwindaji, Mbwa wa chifu Katitu walikuwa mbwa hodari sana kutokana na kuwa n afya nzuri pia kupew mafunzo maalum kwa ajili ya uwindaji. Mbwa walimsaidia katika kazi ya kufukuza wanyama , kuwatisha na hata pia kuwakamata, kitu cha zaidi walichofundishwa hawa mbwa ilikuwa ni kutokula nyama ya mnyama waliyemkamata mpaka pale watakapoluhususiwa na bwana wao ambaye alikuwa ndiye chifu Katitu
Baada ya kuandaa zana na mbwa wake, Chifu Katitu aliwaaga wake zake, chifu Katitu alikuwa na wake watatu, mke mkubwa aliitwa Mwansome, Huyu alikuwa ni mke wa kwanza kuolewa na chifu Katitu na pia alibahatuka kupata watoto wawili. Mke wa pili aliitwa Chambiso, Huyu alikuwa mke wa pili kuolewa na chifu Katitu. Chambiso hakubahatika kupata mtoto. Mke wa tatu alifahamika kwa jina la Bwinsyeho, huyu alikuwa mke mdogo na mke wa tatu kuolewa na chifu Katitu kati ya wake aliokuwa nao, Huyu nae alibahatika kupata watoto wawili.
Baada ya chifu Katitu kuwaaga wake zake, alianza safari ya kwenda msituni akiwa na watumishi wake waaminifu na pia walikuwa hodari kwa shughuli mbalimbali katika utawala wa chifu Katitu , zikiwemo shughuli za mapigano katika jeshi na shughuli za uwindaji. Kutokana na uaminifu na jitihada zao, Chifu Katitu aliweza kuwapa kipaumbele katika kazi mbalimbali za muhimu katika utawala wake, mfano katika mapambano na maadui wa miji jirani, Chifu Katitu aliweza kuwaweka kama viongozi wa vikosi mbalimbali vilivyokuwwa vikienda kupigana na miji iliyokuwa inajaribu kuvamia mji wa Zembilye
Watumishi hodari wa chifu Katitu walifahamika kwa majina kama Chamaka , Yonzebo na Gambiro na pia watumishi hawa kutokana na uhodari wao na uaminifu chifu Katitu aliwaweka kuwa walinzi wake pale alipokuwa nyumbani na hata anatoka kwenda sehemu mbalimbali kama porini kwa ajili ya kuwinda, kwenye vikao na wazee wa kijijini hapo na hata alipoalikwa kwenye sherehe mbalimbali nje ya mji wake
*************************
Zembilye ulikuwa ni mji maarufu sana kiliko miji yote iliyokuwa mpakani mwa mji huu. Umaarufu wa mji wa Zembilye ulitokana na jitihada kubwa za wananchi wake katika kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo na ushirikiano wa wanazembilye katika kutekeleza majukumu hayo ya kijiji na mji wao kiujumla.
Mji wa Zembilye pia uliweza kufahamika na kuwa maarufu kutokana na ubora wa miundombinu yake katika vijiji vilivyokuwa vinapatikana ndani ya mji wa Zembilye. Wanakijiji waliweza kushirikiana katika kutengeneza barabara kubwa zilizokuwa zikiwasaidia katika kusafirisha mazao mbalimbali na nafaka nyingi toka mashambani mwao na kuyapeleka kwenye maghala, majumbani mwao na hata pia sokoni pale kulipokuwa na uhitaji wa fedha. Pia Zembilye ulikuwa mji uliosifika kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali kama vile ng’ombe wa maziwa na nyama , mbuzi wa maziwa na nyama, kondoo, kuku, nguruwe, punda na bata. Ufugaji wa mifugo hii uliwafanya wakulima wa mji wa Zembilye kufanya kazi zao kwa urahisi kama kulima na kubeba mizigo mbalimbali na pia mbolea ya asili iliyofahamika kama samadi, hii ilitokna na kinyesi cha wanyama ambayo wakulima waliitumia kama mbolea wakati wa kupanda mazao na kuwasaidia kuvuna mazao mengi na bora. Wanyama hawa licha ya kuwa na faida kemkem pia waliweza kuuzwa na fedha zilizopatikana zilitumika katika kufanyia shughuli zingine mbalimbali za kimaendeleo
Jeshi imara la mji wa Zembilye ni moja kati ya vitu viliivyoupatia mji umaarufu sehemu kubwa na nyingi pembezoni na mbali ya miji jirani, hii ilitokana na ushindi wa mara kwa mara uliokuwa unapatikana pale walipokuwa wakienda katika vita. Jeshi hili lilikuwa na askari hodari wenye nguvu , ushirikiano na umoja katika shughuli mbalimbali za kijeshi na pia lilikuwa ni jeshi lililokuwa likifanya mazoezi bora kwa ajili ya kujiimarisha katika vita na mapigano yao na maadui zao, Mazoezi yaliyokuwa yamepewa kapaumbele ni kama vile kurusha mikuki kwa mkono, kutumia pinde kurusha mishale , kutumi rungu na mitaimbo
Miji iliyokuwa jirani na mpakani kuuzunguka mji wa Zembilye ilijaribu kutumia kila njia ili kuuvamia mji wa Zembilye lakini “waligonga mwamba”. Chifu Katitu nae aliweza kujigamba waziwazi mbele ya miji jirani iliyokuwa inauzunguka mji wake, Alifanya hivi kutokana na kuwa na jeshi imara lililokuwa likifanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa. Kambi ya jeshi na makao makuu ya jeshi yalikuwa karibu na makazi ya chifu Katitu
*********************************
Taratibu ukubwa wa nyumba za kijijini ulianza kupungua kwa muonekano kutokana na safari ilivyokuwa ikizidi kusonga mbele. Hatimaye wakaanza kuzitazama nyumba za kijijini mithili ya kuchungulia, Hali hii ilionyesha dhahiri umbali waliotembea toka kijijini na wimgi wa miti pale walipoanza kuingia porini. Pori hili lilikuwa jirani kabisa na mji wa Zembilye. Walipozidi kusonga kusonga mbele kidogo waliona kijito kidogo mithili ya mfereji. Kamto haka kalikuwa na maji masafi sana ambayo yalitumika katika kunyweshea mifugo pale ambapo wachungaji wa mifugo walileta mifugo yao katika pori lile, lakini nao pia waliweza kutumia yale maji kwa ajili ya kunywa. Kamto haka kalikuwa na faida kubwa sana kwa wanakijiji hasa wakati wa kiangazi. Hakakuweza kukauka kutokana na wingi wa mito iliyokuwa imesheheni katika msitu ule. Wanakijiji wa mji wa Zembilye walikaweka kakijito haka kama akiba yao ya maji pale ilipotokea shida ya maji wakati wa kiangazi, kwani wakati wa kiangazi visima vya wanakijiji vingi na mito iliyokuwa kijijini iliweza kukauka kutokana na jua kuwaka sana kwa mda mrefu.
***********************
Chufu Katitu alipofika kwenye kajito kale alichota kiasi cha maji na kuyaweka katika mifuko ya ngozi ya ng’ombe iliyokuwa imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuwekea maji na hata pia maziwa, ilitengenezwa kwa kutumia ngozi laini iliyoandaliwa kitaalamu.
Wote walichota maji kwa ajili ya kutumia katika safari yao pale ombapo wangepatwa na kiu au uchovu wa safari.
Baada ya kuchota maji chifu Katitu aliziruhusu mbwa zake zinywe maji, Mbwa walipomaliza kunywa maji, chifu Katitu pamoja na watumishi wake waliendelea na safari yao.
Baada ya safari ndefu kidogo waliweza kuona kichaka kwa mbali kikitikisika, ndipo chifu Katitu alipowaamuru watumishi wake watulie kimya na wachukue tahadhari kwa lolote litakalotokea. Lakini kutokana na uzoefu wa chifu Katitu katika kazi yake ya uwindaji aliweza kugundua kuwa katika kichaka kile panaweza kuwa na kanga wanaotaga mayai wasiopungua watatu, kwani kutokana na kugombania sehemu ya kutagia ndipo husababisha vurugu na kupelekea kichaka kutikisika.
Chifu Katitu na watumishi wake walianza kujongea taratibu kuelekea uelekeo wa kichaka. Chifu Katitu aliwaambia watumishi wake kwa kunong’ona “njoo tukizunguke kichaka hiki ili kanga wasipate nafasi ya kukimbia”. Walipokizunguka kile kichaka kwa haraka na uhodari mkubwa wote waliruka na kutia mikono yao katikati ya kichaka kile, kwa bahati nzuri waliweza kukamata kanga wawili wakubwa na kama chifu Katitu alivyohisi kweli palikuwa na kanga watatu mmoja alifanikiwa kuruka juu na kutokomea mbali. Lakini kwa bahati mbaya walipokuwa wanaluka kuelekea kuelekea kwenye kichaka, mtumishi mmoja wa chifu Katitu aliyeitwa Yonzebo ilichomwa na mwiba mkubwa uliofahamika kwa jina la mchongoma, alichomwa sehemu ya unyayo wake katika mguu. Harakaharaka Yonzebo alitafuta mgomba pori na kuchukua kamba zilizotokana na mgomba huo kasha akajifunga sehemu ile iliyokuwa imepatwa na jeraha ili kuzuia damu isiendelee kutoka.
Baada ya Yonzebo kupatiwa huduma hii ya awali chifu Katitu alitoa mfuko mmoja uliokuwa umetengenezwa kwa kutumia nyuzi za katani,
Kisha akawaweka wale kanga pamoja na mayai sitini yaliyopatikana kwenye kichaka kile, baada ya kuweka katika mfuko alimpatia Chamaka aubebe mfuko uliokuwa umewekwa kanga pamoja na mayai
Waliendelea na safari yao kuelekea ndani zaidi ya msitu mnene uliosheheni kila aina ya mimea na maua yenye harufu nzuri tena mbalimbali na muonekano tofautitofauti unaovutia na usiovutia machoni pa binadamu na wanyama pia.
Katika msitu huu walipatikana wadudu wa kila aina , wanyama mbalimbali wakubwa na wadogo kama vile sungura, cheche, nyati, samba, swala na hata pia panya walipatikana na kila kiumbe ambaye aliweza kustahili kuishi katika mandhali yam situ ule. Hakika pori hili lilikuwa ni msitu mkubwa uliokuwa na kila aina ya kiumbe aliyestahli kuishi msituni.
SURA YA PILI
Wake wa chifu Katitu walipendana sana bila kujari utofauti wao, Wake hawa waliishi kwa furaha. Mke wa pili ambaye hakufanikiwa kupata mtoto aliweza kuwatuma watoto wa wake wenza katika kazi mbalimbali na pia hata hawa watoto licha ya kuwa Chambiso si mama yao lakini walimtii na kumuheshimu kama walivyokuwa wakiwaheshimu mama zao.
Wake wa chifu Katitu mara nyingi walikaa pamoja huku wakiimba pale walipokuwa wamemaliza shughuli zao mbalimbali. Walisaidiana katika kazi za shambani, hata wanakijiji walisifu na kupenda jinsi wake wa chifu wao Katitu walivyokuwa wanaishi kwa kupendana na ushirikiano na kuishi kwa raha, licha ya kuwa na furaha na amani, kulikuwa na vikwazo vilivyotolewa na me wao chifu Katitu. Chifu Katitu hakumpenda mke wa pili, kutopendwa kwa Chambiso kulitokana na kutozaa mtoto hata mmoja tangu aolewe na bwana wake chifu. Kutokana na sababu hii chifu Katitu aliwapenda sana wake wawili mke mkubwa na mke mdogo bkwa sababu walimpatia watoto. Chifu Katitu aliweza kufikia hatua ya kumpiga na kumtukana mkewe wa pili pale tu alipofanya kosa dogo tu, Lakini kutokana na upendo waliokuwa nao wake wa chifu Katitu waliweza kumfariji mwenzao pale tu aliposababishiwa huzuni mme wao na pia walimtia moyo na kumpa tumaini kwamba ipo siku mungu atamsaidia na atabahatika kupata motto na shida zote anazozipata toka kwa chifu Katitu zitatoweka. Chambiso alionekana mtu mwenye furaha siku zote kutokana na kufarijiwa na wake wenzake, hakujari shida anazopata toka kwa mumewe.
Wake wa chifu Katitu walikuwa na hekima isiyokifani, kutokana na hekima yao waninchi hawakusita kupeleka matatizo yao pale ambapo chifu Katitu alipokuwa mbali na himaya yake ndani ya mji wa Zembilye. Kwa ufanisi mkubwa wake wa chifu Katitu waliweza kutatua matatizo ya wakazi wa mji wa Zembilye. Utatuzi huu ulikuwa rahisi kutokana na udogo wa matatizo ya wnanchi wa Zembilye, matatizo hayo kama wizi mdogomdogo na ugomvi kati ya wanandoa na wanakijiji.
***************************
“Bhooooooooo!!........... bhoooooooooo!!................ bhooooooooo!!................” huu ilikuwa ni sauti ya mnyama iliyosikika mita chache toka sehemu waliyokuwepo wawindaji hawa hodari baada ya kutembea kilomita kadhaa toka kwenye kijito ambacho waliweza kuchota maji ya kunywa. “Shiiiiii, shiiiiii, shiiiiii” hiii ilikuwa ni amri na ishara toka kwa chifu Katitu ikwaamuru watumishi wakae kimya. Ndipo wakaanza kujongea taratibu kuelekea kule sauti ilikosikika, Walitembea mithili ya watu wanaotembea ndani ya jumba bovu lisilohitaji bugudha wakihofia kuangukiwa na jumba hilo. Walitembea kimya bila sauti ya aina yoyote kusikika kwani walikuwa wazoefu na kazi hii ya uwindaji.
Kutokana na udhoefu wa chifu Katitu katika uwindaji na watumishi wake, waliweza kuzifahamu aina mbalimbali za sauti za wanyama. Uzoefu huu uliwafanya watambue sauti iliyokuwa imesikika punde, ilikuwa ni sauti ya nyati dume. Kutokana na sifa za wanyama, mmnyama waliyemsikia akipiga kelele aliwafanya wachukue tahadhari ya hali juu. Safari hii Chamaka ndiye aliyekuwa akiwaongoza wenzake mithili ya bata na watoto wake, tofauti na mwanzo pale walipokuwa wanaanza kuingia msituni, kwani hapo awali chifu Katitu ndiye aliyekuwa akiongoza wenzake katika safari yao. Taratibu walisogea mbele kuelekea sehemu ambayo sauti ya mnyama ilisikika, wapili kufuatia katika mstari alikuwa ni chifu Katitu, Gambiro na Yonzebo, Yonzebo alikuwa wa mwisho kwa sababu ya jeraha alilokuwa nalo mguuni katika unyayo, jeraha ambalo lilimfanya awe dhaifu kwa kiasi Fulani katika mawindo
“Kwachu, kwachu, kwachu” nisauti iliyosikika na wawindaji hawa hodari katika msitu. Sauti hii ilisikika umbali Fulani mita kadhaa kutoka kwenye kichaka mbele yao. Kichaka hiki kilikuwa kimestawi vizuri, kikiwa na majani mabichi yaliyovutia kwa chakula cha wanyama wote wala majani. “Jitayarishe” Harakaharaka utekelezwaji wa sauti hii ulianza kutendeka, ilikuwa ni sauti ya chini iliyotamkwa na Yonzebo huku hofu ikimjia kwa mbali kutokana na udhaifu alionao. Alitamka kauli hii baada ya kuona mkia mkubwa wa nyati uliokuwa ukilushwa hewani huku na huko
Uwindaji wa chifu Katitu ulikuwa ni uwindaji wa hali ya juu uliokuwa na kila aina ya mbinu bora za uwindaji, Mara nyingi walifanikiwa katika mawindo yao. Mafanikio hayo yalitokana na mbinu mojawapo waliyokuwa wakiitumia sana mawindo yao, Mbinu hii ilikuwa ni mbinu ya kulusha mikuki au mishale yao kwa pamoja wakikusudia kumpata mnyama yoyote waliyemkusudia kwa wakati huo. Mbinu hii ilitumika mara kwa mara na tena mara nyingi kutokana na kuwa na mafanikio makubwa katika kazi yao ya uwindaji.
Walipokuwa tayarib katika upande wa zana zao kuelekea kule alipokuwepo mnyama, walitega masikio kumsikiliza chifu Katitu. “Moja, mbili, tatu” hii ilikuwa ni sauti ya chifu Katitu ambayo hatima yake ilikuwa ni kuwaruhusu watumishi wake kurusha mishale kutoka kwenye pinde zao kwa pamoja kuelekea uelekeo wa mnyama. Mara tu alipomaliza kuhesabu, mishale ilichoka kwenye pinde zao kwa kasi ya ajabu..................................ITAENDELEA
kwa maoni na ushauri, ufadhili, ntafute kwa
NO ; 0653081338 /
Email ; princekalonga22gmail.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni